IMG-20151017-WA00241 copy
Category: Uncategorized

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Idris Sultan na msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz waliungana kwa kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne ya Mbezi High School, Mbezi ya Kimara Dar es salaam. Idris Sultan na Ommy Dimpozwanashare kitu kimoja muhimu, mastaa hawa wawili walishawahi kusoma shule moja ambayo ndio hiyo Mbezi High School japo miaka tofauti ambapo kwenye mwaliko huu wa mahafali ya kidato cha nne alikuwemo pia Waziri wa habari, utamaduni na michezo, Dr. Fenella Ephraim Mukangara.

IMG-20151017-WA00231 copy

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakaomba picha na mshindi wa Big Brother Africa 2014.

 

IMG-20151017-WA00211 copy

Idris alipewa mic aseme neno na wahitimu wa kidato cha nne wa shule yake, Mbezi High School.