sultan8
Category: Uncategorized

 

Idris Sultan amejipanga kufanya reality show katika kiwanda kikubwa cha burudani duniani Hollywood. Idris kasema tayari show zake mbili zimekamilika ambazo kuna channel kadhaa zitakuwa zikionyesha..amesema itakuwa kama show ya ‘Keeping Up with the Kardashians’ ameamua kufanya kimataifa ili kuangalia soko lake na kupata wawekezaji. Amechanganya Kiswahili na Kingereza na itaanza kuonekana mwishoni mwa mwaka huu. TV Show yake mpya itakuwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia channel ya BET pamoja na channel ya Vuzu za South Africa! Yote ikiwa ni sehemu ya kufanikisha ndoto zake kubwa za kwenda Hollywood, Marekani.

“Kwanza niliwekwa kwenye auditions ambazo nilitakiwa kufanya ili kuingia kwenye Tv show ya ‘The Real Husbands of Hollywood’ show ambayo Kevin Hart yupo, na auditions zangu zilitakiwa zifanyike tarehe 26th April… sasa nikachelewa kuapply Visa ya kwenda USA kwasababu nilikuwa nafanya tours nyingi ndani ya Africa bado kitu kilichopeleka auditions zangu kuwa cancelled, chance hiyo ikanipita na hapo ndipo niliposukunwa sasa kuanzisha reality show yangu mwenyewe ili iwe rahisi kwa mimi kuonekana tena na kupata nafasi nyingine ya kuingia Hollywood…

Reality show hainibadilishi mimi kama mimi kwasababu kwanza haina script, hiyo show itakuwa inaonyesha sana sana ninachokifanya, kwa mfano sasa hivi mnaona tu nafanya vitu tofauti lakini kupitia Reality Show yangu mtakuwa mnaviona ninavyovitimiza, nimevifanyaje, nimepitia nini, na pia muda gani niliwachekesha watu nusu kuzimia… vitu vyote hivi vitaonyeshwa, so kwa ufupi itakuwa inaonesha maisha yangu halisi haswa upande ambao hamuuoni nyinyi kila siku… na haitanipotezea muda bali itakuwa inaonyesha hustle yangu yote na vitu gani ambavyo navifanya mimi kama mimi, na comedy itakuwemo humo humo haitaathiri chochote, comedy zangu zote nitazifanyia humo humo!

Reality Show itaitwa ‘Hustle & Fame’ na hilo jina hatukulipata kirahisi kwa sababu tulihangaika sana kama siku nne hivi tunatafuta tu jina, pia tulikuwa tunatafuta jina la show litakaloendana na uhalisia wa maisha yetu sisi ya kila siku tukiwa tayari maarufu lakini bado tunahangaika…”Idris Sultan